Awali Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza asimamishwe kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo Alhamisi Mei 23, 2019.
Masele alihojiwa na kamati hiyo Jumatatu Mei 20 mwaka huu akituhumiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba amekuwa na utovu wa nidhamu pamoja na kutoa maneno ya kugonganisha mihimili.
Spika Ndugai alilieleza Bunge Mei 16 mwaka huu kwamba kutokana na utovu huo wa nidhamu amesimamisha uwakilishi wa Masele katika Bunge la Afrika (PAP) lililokuwa likiendelea nchini Afrika Kusini na kuagiza mbunge huyo kurejea nchini.