Ndugai kuzindua zoezi la kupima VVU.

In Afya

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo anazindua zoezi la kupima Ukimwi kwa Wabunge kwa hiari.

 

Akizungumza leo, Juni 21, 2018 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na Majibu, Naibu Spika, Tulia Ackson amesema ni vizuri wabunge wote ambao hawajapimwa wakapime Virusi Vya Ukimwi kwa hiari.

“Waheshimiwa wabunge leo Mh. Spika anatarajiwa kuzindua zoezi la kupima virusi vya Ukimwi kwa hiari hapa Bungeni kwa waheshimiwa Wabunge lakini pia na wafanyakazi wa Bunge na atazindua zoezi hilo saa nne leo hii kwenye viwanja vya vilivyopo nyuma ya ukumbi wa Mh. Pius Msekwa,” amesema Dkt. Tulia Ackson.

“Kwahiyo Waheshimiwa Wabunge hasa wale wenye Kamati ya Ukimwi mnaombwa kuhudhuria zoezi la uzinduzi alafu waheshimiwa Wabunge wale wote ambao hawajapima wanaomba kuanzia saa 7 waende kupimwa kwa hiari ili wabunge tuwe tunafahamu afya zetu vizuri.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu