Ndugulile ameshuhudia Ofisi ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu ilivyotelekezwa

In Afya

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameshuhudia Ofisi ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu ilivyotelekezwa na kutojishughulisha na tafiti zozote ndaniya kipindi cha muda mrefu.

Dkt. Ndugulile amebaini hayo Tukuyu mkoani Mbeya wakati wa ziara yake katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu kujionea utendaji wa Taasisi hiyo.

Dkt. Ndugulile ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM kurudisha Tawi la Tukuyu katika hali yake ya awali kama ilivyokuwa ikisifika miaka ya nyuma ikiwa imejikita katika taifiti.

Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM kufanya tafiti zaidi bila ya kutegemea sana wadau kwani zipo fedha za ndani zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya kufanya tafiti zikiwemo tafiti za magonjwa ya binadamu.

Ameongeza kuwa kumekuwa na matatizo mengi ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi ikiwemo kutumia dawa bila kuwa na malaria, UTI na Typhoid ikiwa ni asilimia 70 ya homa zikihusishwa na magonjwa hayo hivyo Taasisi hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya utafiti katika hili na kuwapa majibu wananchi.

“Nimesikitishwa sana na utendaji kazi wa kituo hiki cha Tukuyu na wote naona mmehamia Mbeya nataka nione mabadiliko katika Taasisi hiii hasa kituo hiki cha Tukuyu” alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amemtaka Mkurugenzi wa NIRM kusema kama hawana matumizi ya ofisi ya Tukuyu ili itumike kwa matumizi mengine kwani haoni kinachofanyika katika Taasisi hiyo nyeti katika tafiti za magonjwa ya binadamu nchini iliyopo Wilayani Rungwe.

“Tunataka kukiona hiki kituo kirudi katika heshima yake iliyokuwa nayo siku za nyuma hapa kusiwe ni sehemu ya mapumziko ya watumishi bali kitumike kufanya tafiti”

alisema Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Mkurugenzi NIRM Mbeya Dkt. Nyanda Elias Ntinginya amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa bado wanahiitaji Ofisi ya NIRM Tukuyu kwani bado kuna tafiti zinahitajika ili kuwasaidia wananchi.

Ameongeza kuwa Taasisi hiyo itawakilisha mpango mkakati wa kuiendehsa Ofisi ya Tukuyu ndani ya mwezi mmoja ili kuhakikisha Taasisi hiyoiatekelza majukumu yake ipasavyo katika kuhakikisha inawasaidia kujibu maswali ya wananchi kuhusu magonjwa ya binadamu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu