NEC yaelezwa jimbo la Singida Kaskazini liko wazi.

In Kitaifa, Siasa

Spika wa Bunge Job Ndugai ametangaza kuwa jimbo la Singida Kaskazini lililokuwa likishilikiwa na Lazaro Nyalandu liko wazi baada ya mbunge huyo kufutwa uanachama na CCM.
Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa, Spika Ndugai amemuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi NEC Jaji Semistocles Kaijage kumfahamisha kuwa jimbo hilo liko wazi.
Kwa mujibu wa kifungu 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi 2015 kinaeleza kwamba, pale mbunge atajiuzulu, atakufa au sababu nyingine yeyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113, Spika atamjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali, kwamba kiti hicho cha ubunge kiko wazi.
Kufuatia barua hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaweza kuendelea na mchakato wa kumpata mbunge wa kujaza nafasi hiyo iliyo wazi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu