Neema kuwashukia Watanzania katika mwaka huu wa Fedha.

In Kitaifa

WATANZANIA wameshukiwa na neema katika mwaka huu wa fedha kutokana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupanga kuunganisha mikoa yote nchini kwa kujenga barabara za lami na madaraja.

Bajeti hiyo ni ya Neema pia kwa wakazi wa Dar es Salaam kutokana mkoa huo kupangiwa kiasi kikubwa cha fedha ,kwa ajili ya kujenga barabara za lami nyingi, za viungio na za juu kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari jijini humo, na katika majiji na mji mikubwa mingine.

Bajeti hiyo ya mwaka 2017/18 ya Sh trilioni 4.5 imeweka vipaumbele katika kukamilisha miradi inayoendelea, miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo kwa miaka mitano 2016/17 hadi 2020/21, kutekeleza ahadi za ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2015, na ahadi za viongozi wa serikali walizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka Juzi.

Akisoma bungeni jana, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema, bajeti hiyo ya ukombozi kwa maana ya kuwa inalenga kuunganisha mitandao ya barabara nchini ambayo ni muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda.
Waziri huyo amesema, kati ya fedha hizo, trilioni 2.6 zilizoombwa kwa ajili ya sekta ya uchukuzi, kiasi cha Sh bilioni 900 zitatumika katika kujenga Reli ya Kati sehemu ya Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kiwango cha standard gauge.
Profesa Mbarawa amesema, pia Sh bilioni 500 zitatumika katika kampuni ya ndege, kwa ajili ya kukamilisha malipo ya ununuzi wa ndege tatu ambapo mbili za aina ya CS 300 zenye kubeba abiria 127 kila mmoja na moja ya masafa marefu aina ya Boieng 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 22.
Kuhusu Sekta ya ujenzi iliyotengewa Sh tril 1.9, Prof Mbarawa alisema Sh bilioni 12.8 zitatumika kwa ajili ya kufidia ili kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam- Chalinze Km 144, ujenzi ambao utakuwa wa ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi (

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu