NEYO NA MKEWE CRYSTAL SMITH WAPEANA TALAKA.

In Burudani

Ikumbukwe kuwa taarifa za #neyo kuachana na mke wake #crystalsmith zilianza kama utani mitandaoni baada ya mke wa Neyo kufuta picha za mumewe zote katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Kwa sasa imeripotiwa kuwa wawili hao wameachana rasmi, Neyo amethibitisha katika mahojiano na Podcast ya Private Talk Wikiendi Hii.

Ne-yo amefunguka na kusema kuwa ni kweli wameachana na mpenzi wake Huyo ambaye walifunga ndoa mwaka 2016 na kubarikiwa watoto wawili #shaffer (3) na #roman (Miezi 20) .

Hii imekuja baada ya mkewe kuchapisha kipande cha video katika #InstaStory yake kikimuonyesha akiwa Club huko Chicago na Mwanaume Mwingine, video ambayo ilisambaa zaidi mtandaoni.

Hata hivyo Ne-yo katika mahojiano yake amenukuliwa akisema “Sio kitu cha kusikitisha, ni kitu cha kutambua tu, kufupisha stori sintakuja kumuongelea vibaya, Sio mtu wa hivyo, Ni mwanamke mzuri sana, Ni mama wa watoto wangu wawili atabaki kuwa hivyo” .

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 13 TANZANIA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni

Read More...

CORONA HAITAZUIA KUFANJIKA KWA UCHAGUZI – JPM

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ugonjwa wa Corona hautaizuia Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Rais

Read More...

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani, apandishwa kizimbani

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani Mkami Shirima(30)Mkazi wa Sakina Arusha amefikishwa tena katika mahakama ya hakimu

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu