NITAUNDA KAMATI KUHUSU COVID-19

In Kitaifa

“Suala la Covid 19 nafikikiria niunde Kamati ya Wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya Tafiti za kitaalamu”———Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuwaapisha Viongozi Ikulu Dar es saalam leo

“Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu”———Rais Samia

“Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa”

“TRA nataka muache matumizi ya nguvu na ubabe kwenye kukusanya kodi. Haisaidii. Inaweza kusaidia kwa muda mfupi lalini sio sustainable. Unamkamata mtu unamtwisha kodi ya mabilioni. Halafu unamtishia asipolipa unamfungulia kesi ya uhujumu uchumi. Anaamua kufilisi biashara yake ili akulipe na akwepe kwenda jela. Lakini njia hiyo haiwezi kutusaidia kwa muda mrefu. Mtu hata akikulipa mabilioni ya kodi leo, lakini biashara yake ikafa, kesho mtapata wapi tena kodi? Kwahiyo kakusanyeni kodi lakini si kwa mabavu. Kodi tunazitaka lakini kodi za dhuluma hapana” Rais Samia Suluhu

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Rais Samia Suluhu Hassan atuma salamu za mfungo wa Ramadhani

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewatakia Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Rais Samia Suluhu Hassan,

Read More...

Mourinho alia na VAR kisa kiwiko cha Pogba

Kocha Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho anaamini kwamba kiungo wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba alistahili kuonyeshwa kadi

Read More...

Namungo FC yarejea Bongo tayari kwa ligi kuu bara

Kikosi cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Moroco leo Aprili 12 kimerejea Tanzania kikitokea nchini Zambia ili

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu