Ole aendelea kusikitishwa na kiwango cha timu yake.

In Michezo

MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa hajafurahishwa na uwezo ambao wameonyesha wachezaji wake kwenye mchezo wake wa mwisho kwa kuwa walicheza chini ya kiwango na kuruhusu kufungwa mabao 2-0 na Cardiff.

Manchester United wamemaliza Ligi Kuu England wakiwa nafasi ya sita baada ya kucheza michezo 38 wakiwa wamejikusanyia pointi 66.

“Hatukuwa kwenye ubora wetu, wachezaji wamecheza chini ya kiwango, tumemaliza msimu tukiwa na nguvu kidogo kwa ajili ya msimu ujao.
“Tulikuwa na nafasi ya kumaliza tukiwa ndani ya nne bora, ila michezo yetu miwili ya mwisho tuliboroga na imetugharimu tufike hapa tulipo, kiukweli michezo yetu yote ya mwisho sina uhakika kama tulionyesha juhudi.

“Tulitakiwa tushinde mchezo wetu dhidi ya Huddersfield ila tukalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 hapo ndipo makosa yalianzia hapo, ligi ni ngumu na haijalishi unacheza na nani ni lazima upambane,” amesema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu