Otto Warmbier arejeshwa Marekani

In Kimataifa

Otto Warmbier, mwanafunzi mwenye asili ya Marekani aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, aliyerejeshwa nchini humo wiki iliyopita baada ya miezi kumi na mitano ya kushikiliwa nchini Korea Kaskazini, amefariki dunia siku sita tu baada ya kuachiliwa.

Familia yake imetoa lawama dhidi ya kifo hicho katika kile walichokiita unyanyasaji mkali dhidi ya Otto, aliokuwa akikabiliana nao alipokuwa mikononi mwa maofisa usalama wa Korea Kaskazini .

Akiuelezea utawala wa Korea Kaskazini kama ni wa ukatili mkubwa , Rais wa Marekani Donald Trump ,amesema kwamba Warmbier alikabiliana na mazingira magumu akiwa nchini humo.

Akielezea hali ya kijana huyo amesema alikuwa katika hali ya kutojitambua pindi alipoachiliwa kutoka jela , na kuanzia hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu zaidi karibu na nyumbani kwake Cin cinnati.

 

Madaktari waliokuwa wakimtibia kijana huyo katika hospitali ya chuo kikuu cha tiba mjini humo wamesema kwamba kijana huyo alikuwa na majeraha makubwa ya kuumia neva.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu