Papa Francis awasujudia Kiir na Machar kuhamasisha amani Sudan Kusini

In Kimataifa

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amefanya tendo la unyenyekevu na ambalo halikutarajiwa baada ya kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini, kuwahamasisha kuuendeleza mchakato wa amani.

Mwishoni mwa ziara ya kiroho ya siku mbili ya viongozi hao wa Afrika mjini Vatican, Papa Francis alimuomba rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na hasimu wake Rieck Machar kuendeleza mazungumzo ya amani, licha ya kuongezeka kwa ugumu, na kisha alipiga magoti na kubusu miguu yao, pamoja na ya makamu wa rais Rebecca Nyendeng Garang.

Papa Fransic hufanya tendo la kitamaduni la kiimani la kuwaosha miguu wafungwa siku ya Alhamisi kuu, lakini hajawahi kufanya tendo kama hili kwa viongozi wa kisiasa. Alisema mwishoni mwa ziara hiyo kwamba anataraji kusitishwa kwa uadui, mapigano, mgawanyiko wa kikabila na kurejeshwa kwa hali ya amani nchini humo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu