Picha za Jay-Z na Beyoncé wakiwa kwenye boda boda uswahilini zazua gumzo duniani.

In Burudani, Kimataifa

Kama ni mfuatiliaji wa wasanii wawili wa muziki kutoka nchini Marekani, Beyonce na Jay Z kuanzia jana kwenye mitandaoni ya kijamii kumekuwa na picha za mastaa hao zikisambaa kwa kasi zikiwaonesha wakiwa kwenye boda boda katika maeneo ya uswahilini.

Beyonce na Jay-Z wakiwa kwenye boda boda huko Jamaica

Watu wengi mwanzoni walidhani ni picha za kutengenezwa kutokana na hadhi ya wasanii hao, lakini ukweli ni kwamba picha hizo ni zao na ni za kweli.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail umeeleza kuwa picha hizo za wawili hao wamepiga nchini Jamaica kwenye utengenezaji wa scene ya ziara yao ya kimuziki ya OTR II.

Kwa upande mwingine, mbali ya kutangaza tour yao ya pamoja kwa mara ya pili kuna tetesi kuwa wawili hao huenda wakaachia albamu ya pamoja siku za usoni.

Ziara hiyo ya On The Run II (OTR II) itaanzia katika mji wa Cardiff nchini Uingereza ifikapo Juni 6, 2018 na kumalizika Oktoba 2, mwaka huu katika mji wa Vancouver, nchini Canada ambapo itazunguuka zaidi ya miji 35 duniani.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TCRA yatoa leseni 224 za watoa huduma za maudhui mtandaoni…93 ni za Blogs, 97 ni za Online Tv.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema leseni 224 zimetolewa kwa watoa huduma

Read More...

Muungano wa Afrika umeiomba DR Congo uahirishe kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi mkuu

Muungano wa Afrika (AU) umeitaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iahirishe kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu. Muungano huo unaonuia

Read More...

Bunge kupiga kura tena 29 mwezi januari.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ataitisha kura nyingine Januari 29 kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu