Polisi wamkamata aliyemchinja mkewe na kumuweka kwenye jaba la maji

In Kimataifa

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.

Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa mwandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;

“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.” Ujumbe ulisomeka hivyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu