Prof. Palamagamba ataja mamlaka ya Rais Magufuli Kuhusu Zanzibar.

In Kitaifa
Waziri wa katiba na sheria Profesa. Palamagamba Kabudi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ana mamlaka yote ya kutoa maagizo kwa Mawaziri ambao wapo ndani ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri Kabudi ametoa ufafanuzi huo leo (Jumanne) katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Juma kombo Hamadi alipotaka kufahamu Rais Magufuli ana mamlaka gani kikatiba ya kutoa maagizo kwa Waziri aliyepo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“Rais wa Muungano wa Tanzania anayo mamlaka ya mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi huru”, amesema Prof. Palamagamba.
Pamoja na hayo,  Prof. Palamagamba ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kuwa “katika masuala yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkuu wa nchi ni mmoja tu tena ambaye ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na yeye peke yake ndio Amri Jeshi. Hakuna mtu mwingine yeyote wa kuyaamuru majeshi ya Tanzania isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu yeye ndio kiongozi mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.
Kwa upande mwingine, Prof. Palamagamba amesema Rais wa Zanzibar ni wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwenye heshima na hadhi ya urais kwa mambo yote yasiyokuwa ya Muungano yanayohusu Zanzibar ambapo pia ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi yake hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu