R. Kelly akabiliwa na mashtaka mapya 11 ya unyanyasaji wa kingono.

In Burudani

R.Kelly ameshtakiwa kwa makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Marekani.

Mahakama imeripotiwa kuonyesha kuwa vitendo hivyo vilifanywa dhidi ya watoto wa umri kati ya miaka 13 na 16, na ikiwa itathibitika atakabiliwa na adhabu kali kuliko adhabu nyingine anazokabiliwa nazo.

Mwanzoni mwa mwaka huu msanii huyo wa miondoko ya R&B alikabiliwa na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono. Alikana kuhusuka na vitendo hivyo na akaachiwa huru kwa dhamana.

Ikiwa atakutwa na hatia kwa mashtaka ya awali, yaliyohusisha wanaodaiwa kuwa waathirika wa vitendo hivyo, wakiwemo wasichana wadogo watatu,atakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu mpaka saba gerezani.

Wakili wa R.Kelly Steve Greenberg amesema mashtaka ya sasa si kwamba ni kesi mpya.

”Ameshtakiwa kwenye kesi ambayo bado ipo, ikihusisha watu walewale wanaodaiwa kuwa waathirika na muda uleule (miaka 10 iliyopita) hakijabadilika kitu”, aliandika kwenye ukurasa wa Twitter.

”Mashtaka ni yale yale ni kwamba tu yametolewa kwa nyakati tofauti, wadai ni walewale, muda ni ule ule, ushahidi ni uleule.Tunatarajia matokeo yaleyale.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu