R. Kelly akabiliwa na tuhuma mpya za ulawiti wa kijana wa miaka 17

In Kimataifa

Mwanamuziki wa Marekani wa R&B R. Kelly amekabiliwa na shutuma mpya za kumdhulumu kimapenzi mvulana mwenye umri wa miaka 17 .

Waendesha mashtaka wanadai mwimbaji huyo alimnyanyasa kijana huyo baada ya kukutana naye huko Chicago katika mkahawa wa McDonald’s mnamo 2006.

Wanataka ushahidi wa dhulma hizo na uhalifu mwingine unaodaiwa kutekelezwa naye ambao hakushtakiwa ujumuishwe katika kesi ya Kelly mnamo Agosti.Kelly anakanusha kumnyanyasa mtu yeyote, na mawakili wake hawajajibu madai haya ya hivi karibuni.

Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy, ambaye jina lake halisi ni Robert Kelly, anatarajiwa kushtakiwa New York mwezi ujao kwa mashtaka yakiwemo unyanyasaji wa kingono wa watoto,kuchukua picha mbaya za watoto, udanganyifu na uzuiaji wa haki.

Mashtaka hayo yanahusisha wanawake na wasichana sita ambao hawajatajwa majina.

Sasa, waendesha mashtaka pia wangependa mawakili kusikia juu ya zaidi ya watu wengine kadhaa ambao wanasema Kelly aliwanyanyaswa, kutishiwa au kutendewa vibaya.

Wao ni pamoja na mvulana wa miaka 17 na mwanamuziki mtarajiwa , ambaye Kelly anadaiwa alikutana naye katika McDonald’s na kisha akamwalika kwenye studio zake huko Chicago.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu