Rais atoa agizo kuhusu changamoto za vitambulisho.

In Kitaifa
Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na Ofisi moja pekee ya NIDA.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma
“Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA afike hapa Morogoro ashughulikie hii changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani Watu wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya Gesti,na hili litazamwe Nchi nzima Watu wapewe vitambulisho” amesema.
“Watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na Watu wachache, suala la NIDA linaenda polepole sana, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima”.

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa katika kipindi chake cha uongozi hatopanga bei ya mkulima kuuza mazao yake.

“Wengine wanalalamikia bei ya mahindi kupanda, nataka wakulima washangilie kama bei ya mahindi imepanda, biashara hii lazima iwe huru, bei ya mahindi itajipanga yenyewe, wakati wa kuwapangia bei wakulima kwenye mazao yao umekwisha,” amesema Rais Magufuli.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu