Rais Kenyatta atangaza ukame Kenya

In Kimataifa

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa ukame unaoyakumba maeneo kadhaa ya nchi ya Kenya kuwa janga la Taifa. Kwa mujibu wa serikali, takriban Wakenya milioni mbili kutoka majimbo 10 wanakabiliwa na ukame.

Ameagiza Wizara ya Fedha na Usalama wa Taifa kuongoza juhudi za serikali kuhakikisha kila familia iliyoathirika inapata mahitaji ya msingi.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Msemaji wa Ikulu Kanze Dena Mararo amesema kuwa uamuzi huo, unafuatia mkutano kati ya Kiongozi wa taifa na viongozi 85 kutoka maeneo yenye ukame, wakiongozwa na Waziri wa Fedha Ukur Yatani.

Kwa mujibu wa serikali, takriban Wakenya milioni mbili kutoka majimbo 10 wanakabiliwa na ukame. Hawa ni baadhi ya wakazi wa jimbo la Wajir wanaokabiliwa na makali ya ukame huo.

Wametembea mwendo mrefu kutafuta maji na malisho ya mifugo. Wafugaji wa kutoka majimbo ya Isiolo na Garissa pia wamefika kwenye kisima hiki, hali inayosababisha mzozo, imeripotiwa kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita watu saba wamefariki kutokana na mizozo hiyo.

Taarifa hiyo ya Ikulu imesema, maelezo zaidi yatatolewa kwa umma, ya jinsi ya kuangazia tatizo hilo.

Mwezi uliopita ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu ilielezea mpango wa dharura wa kukabiliana na hali ya ukame. Ukame huo umechangiwa na uhaba wa mvua katika miezi ya Oktoba-Desemba mwaka 2020 na mwezi Machi na Mei mwaka huu kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Mwezi Juni mwaka huu, maeneo mengi ya ukame, yalipata mvua ya wastani wa asilimia 50, iliyosababisha kupungua kwa mazao na mimea katika miezi iliyofuatia.

Asha Mohammed ambaye ni Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya, amesema ni lazima jamii zote ziungane pamoja kuangazia suala hilo.

“Tunajua kuwa kila mtu ana na shida wakati huu, kama sio shida ya chakula ni mahitaji mengine. Watoto wengi wengi wameathiriwa lazima tuone jinsi ya kuwasaidia,” amesema Mohammed.

Shirika la Msalaba Mwekundu linalenga kuzisaidia familia 100,000 katika kipindi cha miezi sita ijayo kwa ushirikiano na mashirika ya serikali katika ngazi za taifa na majimbo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu