Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Madini, Dotto Biteko kuanzisha vituo vya madini kwenye maeneo yanayozalisha migodi nchini.
Ametoa maagizo hayo baada ya kuwaapisha viongozi wapya wa serikali mapema leo Jumatano, Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli ameeleza kuwa maagizo hayo
analenga kudhibiti madini yanayoibwa na kupelekwa nje ya nchi nchi kushindwa kunufaika ipasavyo.
“Sekta ya madini bado ina changamoto kubwa, japokuwa Tanzania tunaongoza kwa kuwa na dhahabu nyingi, bado sio nchi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki ambayo
inaongoza kwa kuuza dhahabu nje,” alisema.
Rais Magufuli aliagiza pia Waziri Biteko kushirikiana na Benki Kuu (BOT) kuweka mkakati utakaowezesha nchi kuanza kununua dhahabu na kuitunza. “Tanzania lazima
isimame, hatuwezi kuendelea kuibiwa dhahabu, lazima tutunze dhahabu yetu, itatufaa hata shilingi yetu ikishuka,” aliongeza.