Rais Magufuli amtaka CAG Kichere asijifanye Mhimili.

In Kitaifa

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemtaka CAG mpya Charles Kichere kutojifanya muhimili, badala yake awe mtiifu kwa mihimili anapoagizwa kutekeleza majukumu.

Bwana Kichere na watumishi wengine walioteuliwa mwishoni mwa juma lililopita wameapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kichere anachukua nafasi ya Profesa Mussa Assad ambaye ameitumikia nafasi hiyo kwa miaka mitano.

Kabla ya wadhifa huu mpya, Kichere alikuwa katibu tawala wa Mkoa wa Njombe.

Akizungumza baada ya kumuapisha, Raisi Magufuli amesema ofisi ya CAG si safi kama inavyofikiriwa.

”Usije ukaenda huko ukajifanya wewe ni muhimili, mihimili ni mitatu tu, na umeiona hapa, mahakama, kuna bunge na sisi wengine wa serikali na katika kiapo chako nilikuwa nakisikiliza nafasi yako ni mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa hiyo mwenye serikali yupo, kafanye kazi zako vizuri za ukaguzi, unapopewa maagizo na mihimili mingine kama bunge katekeleze, usibishane nao ukipewa maagizo na mhimili kama mahakama katekeleze, wewe ni mtumishi”. Alisema Raisi Magufuli.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mourinho kusuka kikosi chake.

Kocha mpya wa Tottenham Jose Mourinho atajaribu kumsajili tena mshambuliaji wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, kutoka Real

Read More...

UNO ya Harmonize yawekwa private, Wasimamizi wa kazi zake waeleza.

Akizungumzia suala la kuripoti YouTube wimbo wa UNO, Magix amesema kuwa alimpa wiki moja Harmonize kumuomba msamaha kwa kutumia

Read More...

Bastola yadondoka na kuuwa mahakamani

Tukio la kusahangaza linalo Treand kwa sasa ni kuhusu kifo cha Mwendesha Mashitaka wa Serikali Afrika Kusini Addelaid Ferreira

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu