Rais Magufuli apiga marufuku michango kwa wanafunzi.

In Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 17, 2018 amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za Serikali za msingi na Sekondari na kuwaagiza Mawaziri Jafo na Ndalichako kusimamia hilo.

 

Magufuli amepiga marufuku hiyo hiyo leo alipokutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka mawaziri hao kwenda kusimamia jambo hilo na kuhakikisha hakuna michango yoyote wanafunzi au wazazi wanachangishwa kwenye shule za sekondari.

 

“Tumesema elimu bure,  haiwezi ikaja kwa mgongo mwingine ikawa elimu pesa. Tumeweka utaratibu kwamba kuanzia shule ya msingi mpka sekondari form four hakuna kulipa ada yoyote lakini sasa hivi michango ya kila aina, nimewapa maelekezo kwamba kuanzia leo iwe ni marufuku na wakalisimamie hili sitaki kusikia mwanachi yoyote mahali popote akilalamika kwamba mtoto wake amerudishwa shule kwa sababu ya michango na walimu wote popote walipo wasishike mchango wowote wa mwanafunzi” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa kama kutakuwepo na mchango wowote wa mzazi ambaye atajisikia kuchangia jambo lolote kuhusu masuala ya shule basi pesa hizo zipelekwe kwa Mkurugenzi na si kushikwa na mwalimu yoyote yule

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu