Rais Magufuli awaonyesha njia Wafanyabiashara.

In Kitaifa, Uchumi
Rais John Magufuli amewatajia  wafanyabishara nchini mambo mawili muhimu akiwataka kutumia fursa za masoko ya ndani ili kukuza ajira na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje.
Akizungumza  jana Jumatatu Machi 19, 2018 katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara Ikulu Dar es Salaam, Dk Magufuli alisema mfanyabiashara yeyote atakayekutana na vikwazo katika uwekezaji huo atoe taarifa mapema na atachukua hatua kwa mteule wake aliyehusika.
Alitoa mfano wa fursa ya kuzalisha sare za wanafunzi na majeshi nchini.
“Tukisema kwa mfano sare zote za wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita zizalishwe na viwanda vyetu vya ndani au tukaanza kuzalisha viatu vya Jeshi, tutashindwa nini,”alisema Rais Magufuli.
Alisema Kiwanda cha Mwatex kitakapoanza kuzalisha sare hizo za wanafunzi, itasaidia kulinda soko la ndani, kuongeza uzalishaji wa zao la pamba na kukuza ajira kwa wakulima.
“Niwaambe Watanzania wenzangu tuwe wazalendo, tukifanya hivyo tutakuwa tumejibu hoja nyingi kwa wakati mmoja, atakayewakwamisha mniambie, mie si ndio mwenyekiti wenu? Ili kusudi nimwambie na yeye akajaribu kufanya biashara,”alisema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TCRA yatoa leseni 224 za watoa huduma za maudhui mtandaoni…93 ni za Blogs, 97 ni za Online Tv.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema leseni 224 zimetolewa kwa watoa huduma

Read More...

Muungano wa Afrika umeiomba DR Congo uahirishe kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi mkuu

Muungano wa Afrika (AU) umeitaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iahirishe kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu. Muungano huo unaonuia

Read More...

Bunge kupiga kura tena 29 mwezi januari.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ataitisha kura nyingine Januari 29 kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu