Rais Magufuli azindua nyumba za Polisi Geita

In Kitaifa

Leo July 15 kutoka Magogo ,Geita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amezindua nyumba 15 za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo Mkoani Geita ambazo zitakuwa na uwezo wa kutumiwa na Askari 30.
Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la polisi chini ya IGP Sirro na kusema jeshi la polisi linachapa kazi achilia mbali changamoto linazokumbanazo,na huku akilisisitiza kuwa makini kwani uchaguzi unakaribia na kuwataka mapolisi watakaobahatika kuishi katika nyumba hizo mpya kuzitunza.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema uzinduzi wa nyumba hizo kwa polisi ni utekelezaji wa ilani wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM ili kuhakikisha wanapolisi wanafanya kazi zao kwa ubora zaidi.

Pia IGP Simon Sirro yeye amesema jeshi la polisi hapa nchini linasimamia maadili pamoja na nidhamu kwa askari wake wote na kusema mpaka sasa tayari jeshi la polisi limewafukuza askari wasiokuwa na heshima na maadili ya kazi takribani 50 huku akihaidi kuwa nyumba za askari nchi nzima zitalindwa vyema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wanavikundi 500 wa kuweka na kukopa kanda ya kaskazini wakutana.

Zaidi ya wanavikundi 500 wa kuweka na kukopa kanda ya kaskazini wamekutana leo jijini Arusha lengo likiwa ni kupata

Read More...

Kijiji cha Ilkeren Kisongo chakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji

Kijiji cha Ilkereni kata ya Kisongo jijini Arusha kinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji jambo linalopelekea wanafunzi wa

Read More...

SERIKALI KUIPATIA BILIONI MBILI KCMC KWA AJILI YA JENGO LA MIONZI

Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuipatia kiasi cha shilingi bilioni mbili

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu