RAIS MAGUFULI AZINDUA SHAMBA LA MITI SILAYO

In Kitaifa

Rais Dk John Magufuli leo amezindua na kubadilisha jina Shamba la Miti Chato na kuliita Shamba la Miti Silayo kama kumbukumbu kutokana na kazi kubwa aliyofanya ya uhifadhi wa misitu hapa nchini.

Dk Magufuli amebainisha hayo wilayani Chato mkoani Geita kwenye uzinduzi wa shamba hilo lenye hekari 69,000.

“Ifike mahali watu wanapofanya kazi nzuri wakumbukwe kwa kazi zao tunapenda mashamba na vitu mbalimbali kuitwa majina ya wanasiasa kwahiyo Prof Dos Santos Silayo nafikiri mamlaka hayo ninayo kwamba shamba hili baada ya kuitwa Shamba la Miti Chato sasa litaitwa Shamba la Miti Silayo” amesema Dk Magufuli.

Dk Magufuli amesema ameamua kufanya hivyo kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na Prof Silayo ambaye ni Kamishana wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) pamoja na vijana maaskari ambao wameendelea kulinda rasilimali za misitu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wananchi Wa Siha Washukuru Serikali Kukabiliana na Nzige

Wananchi wa wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro wameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua kudhibiti makundi ya nzige waliovamia maeneo

Read More...

Wizara Ya Afya Yawataka Wananchi Kuchukua Tahadhari Dhidi ya COVID – 19

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasihi na kuwasisitiza zaidi wananchi kuzingatia tahadhari zote ikiwemo

Read More...

Ndege mbili kupambana na nzige Longido

Serikali nchini imetangaza kuanza kutumia ndege kunyunyizia dawa makundi ya nzige yaliyovamia wilaya ya Longido na Simanjiro wakitokea

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu