Rais Magufuli leo ameagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

In Kitaifa

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo Januari 3, 2018 ameagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anayemaliza muda wake Prof. Benno Ndulu Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo yao, Prof. Ndulu amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kufanya naye kazi tangu alipoingia madarakani na amebainisha kuwa anafurahi kumaliza kipindi chake huku uchumi wa nchi ukiwa mzuri.

Aidha Prof. Ndulu amempongeza Rais Magufuli kwa miongozo muhimu iliyosaidia kuimarisha uchumi ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei ambao mwezi Novemba 2017 ulifikia asilimia 4.4 na kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani Bilioni 1.8 hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 6 hivi sasa, hali ambayo imeimarisha uwezo wa Serikali kujiendesha na kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo.

Aidha Rais Magufuli amezungumza na Gavana Mteule Prof. Florens Luoga na baada ya mazungumzo hayo, Prof. Luoga amemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi huo na kumhakikishia kuwa ataisimamia BoT ili iendelee kuwa chombo imara cha kusimamia uchumi wa nchi, kusimamia fedha ya Tanzania na kuhakikisha nchi inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu