Rais Magufuli akamilisha ziara yake.

In Kitaifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Jana Julai 25 ,amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kwa kufungua barabara ya Itigi – Manyoni Mkoani Singida.
Barabara hiyo inayounganisha Mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma ina urefu wa kilometa 89.3 na imejengwa gharama ya Shilingi Bilioni 114.692, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza na wananchi wa Itigi katika sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, amesema Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa barabara hiyo pamoja na nyingine saba alizozifungua, katika ziara hii zenye urefu wa jumla ya kilometa 707 zimejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 806, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Rais Magufuli amebainisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, na kwamba Serikali imeamua kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini kwa lengo la kuhakikisha barabara za vijijini zinajengwa kwa kiwango cha lami.
Kwa barabara ya Mkiwa – Itigi yenye urefu wa kilometa 57 na ambayo tayari zabuni ya ujenzi ilishatolewa kwa mkandarasi ili aijenge kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 104, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuupitia upya mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa kiwango cha fedha kilichopangwa ni kikubwa ikilinganishwa na gharama halisi.
Pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa kujadiliana na Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili aweze kuendelea kujenga barabara kutoka Itigi kuelekea Chunya hadi Makongorosi Mkoani Mbeya.
Viongozi wengine waliongozana na Mhe. Rais Magufuli katika ziara ya leo ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King na Wabunge wa Mkoa wa Singida.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu