RAIS MPYA WA MPITO SUDAN AAPISHWA.

In Kimataifa

Luteni Jenerali Awad Ibn Auf ameapishwa kuwa kiongozi wa Baraza la kijeshi la Mpito kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kutangaza kuondolewa jana kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 35, Omar al -Bashir.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuapishwakwa kiongozi huyo wa mpito, Mmoja wa kiongozi wa Baraza la Utawala wa Kijeshi la mpito, Luteni Jenerali Omar Zain al Abidin amesema, jukumu kubwa lililo mbele yao ni kusimamia masuala yote ya umma.

Luten Jenerali huyo amesema, katika kipindi hicho cha mpito hawatakuwa na uvumilivu katika vitendo vyovyote vibaya vitakavyojitokeza popote pale ndani ya nchi hiyo.

Katika hatua nyingine, Umoja wa Afrika (AU) umesema kuwa utawala wa Kijeshi siyo suluhisho la matatizo na changamoto zinazoikumba nchi ya Sudan, na wale siyo matamanio ya raia wake waliokuwa wakiandamana kuipinga Serikali ya Rais Omary al –Bashir.

Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Luteni Jenerali Ahmed Awad Ibn Auf kutangaza kuwa Jeshi litaunda serikali ya mpito ambayo itaongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili,

Mbali na Serikali hiyo, Luteni Jenerali Ahmed ambaye alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Rais Bashir amesema kuwa wamesimamisha Katiba sambamba na kutangazwa kuwa na hali ya hatari kwa miezi mitatu ambayo wananchi hawatatakiwa kuwa nje baada ya saa tatu usiku.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu