Rais Mugabe achangia dola milioni 1 kwa kuuza ng’ombe.

In Kimataifa

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amechangia Umoja wa Afrika (AU) dola za kimarekani milioni 1, baada ya kuuza mamia ya ng’ombe nchini kwake.

Kiongozi huyo amesema kuwa alitoa ng’ombe 300 lakini Wakulima wa Zimbabwe walimuunga mkono na kutoa mara mbili ya idadi hiyo, lengo likiwa kuisadia AU kuondokana na utegemezi wa nchi za Magharibi.

Mugabe alikabidhi hundi ya $1m kwa AU katika mkutano wa viongozi wa Umoja huo uliofanyika nchini Ethiopia, mwanzoni mwa wiki hii.

Mugabe mwenye umri wa miaka 93, wakati akiikabidhi hundi.

Amesema  Kama mkulina na Muafrika, kuchangia ng’ombe ni ishara ya mali, huja kiasilia tu na  suala la AU kujiwezesha kufanikisha shughuli zake yenyewe imekuwa agenda muhimu zaidi katika vikao vya hivi karibuni vya Umoja huo.

Agenda hiyo ilianzishwa kwa nguvu katika mkutano wa 27 wa wakuu wa nchi wanachama uliofanyika jijini Kigali nchini Rwanda, mwaka mmoja uliopita.

Zimbabwe ambayo ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la kiuchumi na upungufu wa chakula, mwaka huu umekuwa wa neema kwake kwani nchi hiyo inatarajia mavuno mazuri kulinganisha na miaka iliyopita.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu