Rais Samia akutana na Mstaafu wa Nigeria Obasanjo

In Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo May 3, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma ambapo Rais Mstaafu Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia kufuatia vifo vya waliokuwa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Hayati Benjamin William Mkapa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli waliofariki dunia tarehe 23 Julai, 2020 na tarehe 17 Machi, 2021 mtawalia.

Rais Mstaafu Obasanjo amempongeza Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake.

Aidha, katika mazungumzo hayo viongozi hao wamezungumzia hali ya usalama Barani Afrika na umuhimu wa Wakuu wa Nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro hiyo ambayo inasababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto.

Pia viongozi hao wamezungumzia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu