Rais Shein afanya uteuzi

In Kitaifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:

  1. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
    i. Bwana Iddi Haji Makame ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika Wizara ya Fedha na Mipango.

ii. Bwana Khatib Mwadini Khatib ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango.

iii. Dkt. Suleiman Simai Msaraka ameteuliwa kuwa Kamishna wa Bajeti katika Wizara ya Fedha na Mipango.

iv. Bwana Ame Burhan Shadhil ameteuliwa kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali katika Wizara ya Fedha na Mipango.

  1. WIZARA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

i. Bibi Asha Zahran Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mifugo katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.

  1. WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

i. Bibi Rahima Ali Bakari ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) katika Wizara ya Biashara na Viwanda.

  1. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

i. Bwana Mohamed Habib Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji katika Kamisheni ya Ardhi.

ii. Bwana Mtambua Hamziji Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ardhi katika Kamisheni ya Ardhi.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 5 Februari 2020.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Hospitali Ya Wilaya Karagwe Yakamilika Kwa 98%

SERIKALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imetumia sh. bilioni 1.8 kujenga majengo mbalimbali ya hospitali ya wilaya ya Karagwe

Read More...

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine TAWIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Eblate Ernest Mjingo kuwa Mkurugenzi Mkuu

Read More...

Tamisemi Yakanusha Taarifa Iliyotolewa Na Mgombea Urais Wa Chadema,tundu Lissu

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imekanusha madai yaliyotolewa na mgombea urais wa Tanzania

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu