Rais Trump akutana na Malkia Elizabeth wa Uingereza.

In Kimataifa

Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na Malkia Elizabeth wa Pili nchini Uingereza alikokwenda kwa ziara ya siku mbili ya kiserikali yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Hata hivyo, ziara hiyo inagubikwa na mvutano wa Brexit pamoja na malumbano ya kisiasa kati ya Trump na meya wa jiji la London. Rais Trump na mkewe Melania walifika kwenye kasri la Buckingham kwa kutumia helikopta na kupokelewa na mrithi wa ufalme Charles na mkewe Kamilla. Maelfu ya watu wakiongozwa na makundi ya wanawake wanapanga kufanya maandamano makubwa karibu na uwanja wa bunge kesho Jumanne wakati rais huyo wa Marekani atakapokutana na Waziri Mkuu Theresa May na viongozi wa Marekani na kibiashara. Ziara ya kiongozi huyo wa Marekani imefunikwa na ujumbe wake wa Twitter aliouandika akimtukana Sadiq Khan ambaye ni meya wa kwanza Muislamu wa jiji la London.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu