Rais wa Algeria atangaza kuwania muhula wa tano madarakani.

In Kimataifa

Rais wa Algeria ambaye pia amedhoofika kiafya Abdelaziz Bouteflika amesema anatarajia kugombea awamu ya tano ya urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi wa April. Taarifa hiyo imesema rais Bouteflika mwenye miaka 81, aliyeko mamlakani tangu mwaka 1999, ametangaza kugombea kwenye ujumbe wake alioutoa jana Jumapili. Bouteflika alipatwa na kiharusi mwaka 2013, na tangu hapo amekuwa akionekana mara chache hadharani. Tangazo hili linakuja siku moja baada ya chama tawala cha Algeria cha National Liberation Front kumtangaza Bouteflika kugombea. Ni rais pekee wa Kaskazini mwa Afrika aliyenusurika katika vuguvugu la mapinduzi ya umma katika ulimwengu wa Kiarabu lililoanza katika nchi jirani ya Tunisia. Anaheshimika nchini humo kwa kukomesha vita ya wenyewe kwa wenyewe ya taifa hilo baina ya wanamgambo wa Kiislamu na jeshi iliyowaua watu takribani 200,000.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

David Luiz kuitangaza Rwanda Kimataifa.

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, David Luiz ameahidi kuitangaza Rwanda kimataifa kwenye sekta ya utalii kwa marafiki zake wanaoishi

Read More...

Rekodi yawekwa na Kipchoge kutoka Kenya

Eliud Kipchoge amekuwa Mwanariadha wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini

Read More...

Habinder Seth aandika barua kwa DPP kukiri makosa yake.

Habinder Seth, anayekabiliwa na makosa ya Uhujumu Uchumi amemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kukiri makosa yake na

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu