Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na wa Uganda waweka mikakati ya kushirikiana.

In Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi amekuwa katika ziara ya siku mbili nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kibiashara wa mwaka 2019.

Wizara ya mambo ya nje nchini Uganda imetoa maelezo kuwa wakuu wa mataifa hayo mawili walikutana ili kukamilisha mkakati wa kushirikiana katika masuala ya afya, amani na usalama, nishani ,biashara na uwekezaji pamoja na masuala mengine ya maendeleo.

Katika suala la usalama na amani ambayo ni changamoto kubwa kwa mataifa hayo mawili, viongozi hao wameazimia kutafuta suluhu ya kuyangamiza makundi ya wapiganaji na waasi mashariki mwa Kongo.

Marais hao wanamini kuwa hiyo ndiyo itakuwa hatua ya kwanza kuleta maendeleo ya viwanda, biashara na uwekezaji eneo hilo.

Viongozi hao wametoa mwito kwa wenzao katika kanda ya maziwa makuu kuunga mkono juhudi zao.

Baada ya kukutana kwa siku nne, ujumbe wa DRC uliojumuisha maafisa wa ngazi za juu pamoja na wawakilishi 110 wa wafanyabiashara, waliorodhesha na wenzao wa Uganda masuala ambayo waliyataka viongozi wayazingatia ili kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Kipchoge anatarija kupokea taji la BBC la mwanaspoti bora

Mfalme wa mbio za Marathon Eliud Kipchoge anatarija kupokea taji la BBC la mwanaspoti bora wa mwaka rasmi

Read More...

Jerry Muro akabidhi kituo cha kisasa kwa ajili ya ukaguzi wa magari ya utali

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro amekabidhi kituo cha kisasa kwa ajili ya ukaguzi wa magari

Read More...

RANCHI YA MISSENYI YATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO KWA KUIMARISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZILIZOPO.

RANCHI YA MISSENYI YATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO KWA KUIMARISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZILIZOPO. Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu