Rais wa mpito wa Algeria Abdelkader Bensalah ameahidi kuandaa uchaguzi huru katika siku 90

In Kimataifa

Rais wa mpito wa Algeria Abdelkader Bensalah ameahidi kuandaa uchaguzi huru katika siku 90 zijazo kufuatia wiki za maandamano ambayo yalisababisha kujiuzulu Rais  Abdelaziz Bouteflika baada ya kuwa madarakani kwa miaka 20.

Bensalah mwenye umri wa miaka 71 alikataliwa na waandamanaji mara tu alipotangazwa na bunge kuchukua usukani wa nchi katika kipindi tete cha mpito baada ya miongo ya utawala wa kimabavu.

Kwenye hotuba yake ya televisheni, Rais huyo wa mpito amesema ataunda tume ya huru ya kitaifa itakayosimamia mchakato wa uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki.

Bensalah amesema jeshi la nchi hiyo litahakikisha amani inadumishwa kwa ajili ya watu wa Algeria huku akiahidi kuwa atashauriana na viongozi wa kisiasa na asasi za kiraia kwa ajili ya kuamua mustakabali wa taifa hilo la Afrika ya Kaskazini.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

CAF YAWAPIGA CHINI MAREFA WA TANZANIA AFCON 2019, YACHUKUA HADI WA BURUNDI,KENYA,TANZANIA HOLAA.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya marefa 27 na marefa wasaidizi 29 kwa ajili ya Fainali za

Read More...

Man U, Juventus wafungishwa virago UEFA

Timu ya Manchester United imeondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya hatua ya robo fainali baada ya kukubali

Read More...

Arsenal yarejea nafasi ya nne ligi kuu.

Arsenal yafanikiwa kurejea tena nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya premia baada ya ushindi wake dhidi ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu