Rais wa Sudan Kusini ametangaza hali ya hatari kwa muda wa miezi mitatu katika jimbo la Gogrial.

In Kimataifa

Rais Salva Kiir  wa Sudan Kusini ametangaza hali ya hatari kwa muda wa miezi mitatu katika jimbo la Gogrial, ambako mapigano yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa, kati ya wanamgambo kutoka koo za Apuk na Aguok za kabila la Dinka, analotokea Kiir.

Msemaji wa serikali amesema hapo jana.

Michael Makuei, ambaye pia ni waziri wa habari, amesema jeshi litapewa mamlaka maalum kuzuia mapigano katika jimbo hilo la Gogrial, na kwamba haki za raia zitasitishwa, licha ya kwamba rais hajatangaza ni haki gani zitaathirika.

Makuei alisema watu wapatao 70 waliuawa katika mapigano ya mwezi Mei.

Makuei amesema hali ya hatari pia inahusu katika maeneo jirani ya Tonj, Wau na Aweil mashariki.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu