Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya Uteuzi wa Wakuu wa mikoa wawili.

In Kitaifa

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  amefanya mabadiliko ya Uteuzi wa Wakuu wa mikoa wawili. 

John Mongella aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. David Kafulila aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, Mei 19, 2021 wakati akihutubia mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa na wakuu wa taasisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Kuna mabadiliko madogo nimefanya, Kafulila nilimteua kuwa RC Arusha na Mongella kuwa RC Simiyu, nimeamua Mongella kwa sababu ulikuwa unaongoza Mkoa mkubwa basi ukawe RC Arusha na Kafulila kwa sababu ndio anaanza alikuwa RAS basi akawe RC Simiyu.

“Wote mlioapa na mlioteuliwa hongereni sana, nasema hongereni kwasababu Tanzania kuna Watu wengi na 15% wangefaa kuteuliwa lakini mmeteuliwa nyinyi, naamini mnapokwenda kufanya kazi zenu mtasimama na Mungu.

“Baada ya shughuli hizi za kuapishana na kupiga picha Wakuu wa Mikoa na Wateuliwa wengine mtarudi hapa na tutakuwa na kikao cha kazi kwahiyo kwasababu nina mambo mengi ya kuongea na nyinyi leo tuishie hapa tutakutana kwenye kikao cha kazi,” amesema Samia.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake 5 wafikishwa mahakamani kwa makosa matano ikiwemo

Read More...

George Mkuchika Aaapishwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum.

Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Kampeni Mstaafu George Mkuchika kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum. Kabla ya

Read More...

Waziri wa Uganda ajeruhiwa na mwanae kufa baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Watu wenye silaha wamemshambulia na kumjeruhi Waziri na Kamanda wa zamani wa jeshi la Uganda, na kumuua binti yake

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu