Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Kenya kwa ziara rasmi ya ya siku mbili.
Ziara hii ya rais Samia ni muendelezo wa jitihada za nchi hizo mbili kuboresha na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na itakuwa ndio ziara ya pili nje ya taifa lake kwa rais Samia tangu alipochukua madaraka kutoka kwa hayati Dkt John Magufuli.
Rais Samia anatarajia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili.
Wizara ya Mambo ya Nje TanzaniaCopyright: Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania
Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi.
Alifanya safari yake ya kwanza akiwa Rais nchini Uganda mnamo Aprili 11 na Rais Yoweri Museveni akielezea kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda
Rais huyo ameonekana kutopendelea kulinganishwa na Magufuli na amewashutumu wabunge wa Tanzania kwa kufanya hivyo.