Rais wa Urusi atoa pongezi kwa timu ya Taifa.

In Michezo

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameipongeza timu ya taifa hilo kwa kupata ushindi dhidi ya Hispania na kujihakikishia kusonga mbele mchezo wa michuano ya kombe la dunia inayoendelea kwenye nchi hiyo mwaka huu 2018.

Urusi ambayo ni mwenyeji wa michuano hiyo imeingia huku ikionekana kuwa timu dhaifu lakini imeweza kufanya maajabu makubwa mpaka sasa baada ya kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Saudi Arabia na Misri mpaka inatinga hatua ya robo fainali.

Timu hiyo ambayo imepata mafanikio makubwa mpaka sasa ya Urusi imehudhuriwa mara moja wakati wa ufunguzi na rais wa nchi hiyo wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo ya FIFA.

Putin ameshindwa kuhudhuria kwenye mechi dhidi ya Hispania iliyopigwa kwenye dimba la Luzhniki jijini Moscow kwa sababu ya majukumu ya kiserikali yanayo mkabili.

Kwa mujibu wa msemaji wake, amesema kuwa Putin alimuita meneja wa kikosi cha Urusi, Stanislav Cherchesov kabla ya mechi na kumtakia kilalakheri na hata baada ya mchezo huo alimpa pongezi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu