Rais wa zamani wa argentina, afunguliwa mashitaka ya rushwa.

In Kimataifa

Rais wa zamani wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner amefunguliwa mashitaka ya rushwa, siku tatu baada ya kutangaza kuwania nafasi ya makamu wa rais katika uchaguzi wa Oktoba. Kirchner anatuhumiwa kwa kumpendelea mfanyabiashara Lazaro Baez ili kupatiwa zabuni za umma zenye thamani ya mamilioni ya dola wakati akiwa rais mwaka 20017-2015.Mfanyabiashara huyo anayetokea jimbo la Santa Cruz ambako ni ngome ya Kirchner, anahisiwa kuanza kupata upendeleo wa aina hiyo wakati Nestor Kirchner ambae ni mume wa Cristina alipokuwa rais kati ya mwaka 2003 hadi 2007. Waendesha mashitaka wamesema zabuni zilitolewa kwa gharama ya juu mno na kusababisha miradi mingine kukwama. Kirchner pia anakabiliwa na mlolongo wa uchunguzi wa madai ya ufisadi, lakini haya ni ya kwanza kufikishwa mahakamani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu