Ramaphosa asema ghasia za sasa hazijawahi kushuhudiwa

In Kimataifa

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema ghasia zilizosababisha mauaji nchini humo hazijawahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Machafuko hayo yamesababishwa na maandamano ya wiki nzima kupinga hatua ya rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kufungwa miezi 15 gerezani. Akilihutubia taifa jana usiku, Ramaphosa amesema baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini yanakabiliwa na siku kadhaa za vurugu, uharibifu wa mali na uporaji ambao haujawahi kutokea katika historia ya demokrasia ya nchi hiyo.

Ramaphosa amesema ghasia hizo zimevuruga mpango wa kutoa chanjo ya virusi vya corona na kwamba zitazidisha umasikini, kukosekana kwa ajira na watu kupoteza maisha. Watu 10 wameuawa, wengine wakiwa na majeraha ya risasi waliyopata baada ya jeshi kupelekwa kwenye maeneo kadhaa ya nchi. Watu 489 wamekamatwa. Ramaphosa amesema aliamuru jeshi lipelekwe kuwasaidia polisi kukabiliana na waandamanaji.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu