RAPPA G-EAZY NA MEGHAN THE STALLION KWENYE MAHABA MAZITO.

In Burudani

Mwezi wa wapendanao umeanza vizuri kwa rappa wa kimarekani #GEazy na mwanadada anayefanya vizuri kwa sasa katika kiwanda cha muziki wa Hip Hop #MeghanTheStallion baada ya kuiteka mitandao ya kijamii hiyo jana kwa video fupi ambayo ilisambaa kila kona ikiwaonyesha wawili hao wakiwa katika huba zito.

Bado hakuna aliyethibitisha taarifa za wawili hao kutoka kimapenzi lakini video iliyochapishwa jana katika #InstaStory ya rappa Eazy na baadae kuja kuifuta baada ya kuona imesambaa inaonyesha wazi kuwa wawili hao wapo katika penzi zito.

Ikumbukwe kuwa Eazy aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanadada anayefanya vizuri katika muziki wa #rnb #halsey ambaye hawakudumu sana licha ya kuwaachia mashabiki zao ukumbusho wa nyimbo ya pamoja iitwayo Him And I.

Tangu jana mashabiki wameendelea kujiuliza nini ambacho kimemvuta rappa huyo kwa Meghan binti mwenye asili ya Kiafrika huku wengi wakitarajia kumuona Eazy katika kampani na wamarekani weusi.

Hata hivyo Meghan alikua kwenye mahusiano na rappa #MoneyBaggYo ambaye mpaka sasa aijulikani wameachana au la kutokana na kutoonekana tena wakiwa pamoja tangu mwanadada huyo atoe wimbo wake aliomshirikisha #NickMinaj Hot Girl Summer.

Hivyo inaonekana wazi kuwa Eazy ana nafasi kubwa ya kufia kwenye majeshi ya binti huyo wa kimarekani mwenye shepu la kitanga.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TUME YA MADINI KWENYE MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika

Read More...

Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokomeza mimba za utotoni.

Halmashauri ya Jiji la Arusha ikishirikiana na wataalamu wa Afya kutoka mashirika mbalimbali, maafisa  elimu kata na sekondari,

Read More...

MNADA WA ALMASI WDL WAZIDI KUPAMBA MOTO.

Leo tarehe 20 Februari, 2020 mnada wa asilimia tano ya madini ya almasi kutoka katika Mgodi wa Williamson Diamond

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu