RC Makonda Aagiza Kukamatwa Kwa Vigogo Waliohujumu Soko La Kariakoo.

In Kitaifa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa waliokuwa viongozi wa Soko la Kimataifa Kariakoo kwa kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3.
Vigogo walioagizwa kukamatwa ni aliekuwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya utumishi, mkuu idara ya manunuzi na aliekuwa mkuu idara ya mipango na biashara ambao wameagizwa kufikishwa mahakamani Mara moja.
RC Makonda ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa utatuzi wa kero za wafanyabiashara Soko la Kariakoo ambapo pia ametoa siku tano kwa watendaji kupitia upya sheria zote za ushuru mdogomdogo baada ya kubaini uwepo wa ushuru mkubwa unaoumiza na kuwarudisha Nyuma wafanyabiashara.
“Hatuwezi kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha Nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo 600, ushuru wa Siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyohuyo analipa ushuru wa Choo na Bafu 500, hili haliwezekani” Alisema RC Makonda.
Aidha RC Makonda ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa makusanyo ya ushuru baina ya mbia na soko na badala yake ameagiza kazi ya ukusanyaji wa ushuru ifanywe na uongozi wa soko.
Pamoja na hayo RC Makonda ameagiza soko kuu la kariakoo kurejeshwa kwenye hadhi ya kimataifa na sio kuendeshwa kiholela Kama ilivyo sasa ambapo linapokea bidhaa za rejareja kutoka mitaani badala ya kuwa soko la kuuza bidhaa za jumla.
Miongoni mwa kero zilizolalamikiwa na wafanyabiashara ni uhusiano mbovu baina ya viongozi na wafanyabiashara, kodi ya pango, vyanzo vingi vya ushuru, mikataba, mikopo, soko kupoteza mwelekeo, mkanganyiko kwenye viwango vya vipimo, kadi ya kizimba na ukamataji ambapo RC Makonda ameahidi kuzifanyia kazi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu