RC Makonda ataka shule zifungwe kwa masaa 72.

In Kitaifa

Mkuu wa Dar es salaam, Paul Makonda ameziomba Mamlaka za Elimu kufunga shule kwa siku mbili kufuatia mvua zinazoendelea katika jiji hilo.

RC Makonda ameyasema hayo leo wakati akikagua maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Dar es salaam.

“Nimeziona Mamlaka za elimu kufunga shule kwa siku mbili, hadi tutakapowaambia siku ya Jumatano kulingana na hali itakavyokuwa kwasababu mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi yamejaa mengi kwa hali hii sio salama,” amesema RC Makonda.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa akiongea na Bongo5 amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema kuwa watu sita wameripotiwa kufariki katika wilaya za Kinondoni na Ilala huku mmoja akiripotiwa kufariki katika wilaya ya Temeke.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu