RC Makonda atoa taarifa kuhusu tukio la kushambuliwa kwa afisa ubalozi wa Syria.

In Kitaifa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ameshtusha na taarifa zilizosambaa mitanaoni kuhusu tukio la Afisa mmoja wa Ubalozi wa Syria ambaye amedaiwa kushambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha.


Afisa wa Ubalozi wa Syria anayetajwa kushambuliwa na kuporwa fedha

Mhe. Makonda ametoa taarifa yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa ambapo amewataka wananchi kutulia na vyombo vya usalama wanafuatilia kwa umakini tukio hilo.

Soma taarifa hiyo hapa chin:

TAARIFA YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA AFISA UBALOZI WA SYRIA.

Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha leo mchana Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini zaidi.

Nawaomba sana wananchi wa Dar es Salaam muendelee kuwa watulivu na mkielewa kwamba Mkoa wenu ni salama salama sana. Vyombo vya usalama vinalifanyia kazi tukio hili na taarifa za awali nilizopokea zinaonyesha tukio hili linaweza kuwa limepangwa na watu wa ndani. Tunafuatilia zaidi kujua kwa nini Afisa huyo hakuomba ulinzi wa polisi akiwa amebeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na pia kwa nini dereva wake amekimbia.

Kwa hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano ikawa ni tukio la kupangwa na watu wa ndani. Hatutaruhusu watu wachache wachafue taswira ya Mkoa wetu.

Uchunguzi ukifikia sehemu nzuri taarifa rasmi itatolewa na vyombo vyetu vya usalama. Ulinzi na usalama wa wananchi wetu ni muhimu sana.

Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu