RC Makonda Atokwa Na Chozi, Ni Baada Ya Kujionea Maisha Ya Wastaafu Waliodhulumiwa Nyumba

In Kitaifa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana  ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.

RC Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote.
Story ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyohuzunisha kuona mnyonge anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu  anamdhulumu Mali yake.
Makonda amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Bank, Muuzaji wa nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi.
Kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha.
Kwa upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia kitendo cha RC Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa utendajikazi wa RC Makonda wanapata haki yao.
Aidha wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi wanyonge.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu