Rekodi yawekwa na Kipchoge kutoka Kenya

In Kimataifa, Michezo

Eliud Kipchoge amekuwa Mwanariadha wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili.

Raia huyo wa Kenya alikimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria hii leo.

Haitatambulika kuwa rekodi mpya ya dunia katika mbio hizo kwa kuwa halikuwa shindano la kila mtu mbali na kwamba alitumia kundi la wanariadha wa kusukuma kasi waliokuwa wakishirikiana naye na kutoka.
Bingwa huyo wa dunia katika mbio ndefu alikuwa akishangiliwa kila upande na watu waliofika kumshuhudia.

#Radio5michezo
#Theonlychoice

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu