Ripoti ya UNICEF yaonesha ndoa za utotoni zimepungua duniani.

In Kitaifa

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo Machi 06, 2018 Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto ulimwenguni ( UNICEF) limesema kuwa kuna mafanikio makubwa ya kupungua kwa ndoa za utotoni duniani.

Tokeo la picha la ndoa za utotoni

UNICEF wamekadiria kuwa ndoa za utotoni zipatazo milioni 25 zimeweza kuzuiliwa kwa kipindi cha muongo mmoja uliyopita.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa msichana mmoja kati ya watano anaolewa chini ya miaka 18 tofauti na miongo iliyopita ambapo ilikuwa msichana mmoja anaolewa kati ya wanne.

UNICEF wamesema bara la Asia hususani Asia ya Kusini limejitahidi zaidi katika kupunguza ndoa za utotoni, ambapo ripoti imesema wamepunguza kwa asilimia 20 kutoka 50 iliyokuepo miaka 10 iliyopita.

Mshauri wa masuala ya jinsia kutoka UNICEF, Anju Malhotra amesema kuwa mabadiliko hayo ni kutokana na sera nzuri za serikali ikiwemo elimu kwa watoto juu ya ndoa za utotoni.

“Kama msichana atalazimishwa kuolewa akiwa mtoto, atkabiliwa na madhara makubwa siku za usoni. Kwani itakuwa ni kikwazo kwa kupata elimu pia ni rahisi kudhalilishwa na mumewe na inahatarisha maisha kipindi cha kujifungua. Mbaya zaidi ndoa za utotoni zina madhara makubwa kwenye jamii ikiwemo umasikini.”amesema Bi. Malhotra.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa nguvu kubwa ya kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni imehamia barani Afrika,ambapo jitihada za ziada zinahitajika ili kupunguza tatizo hilo.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu