Roma aomba kupunguziwa adhabu.

In Burudani, Kitaifa

Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amefunguka kwa mara ya kwanza ikiwa ni mwezi mmoja toka afungiwe na Baraza la Sanaa la Taifa kujihusisha na shughuli za sanaa kutokana na kudaiwa kutoa wimbo ‘Kibamia’ ambao hauna maadili.

Basata wamesema walimfungia msanii huyo baada ya kutakiwa na baraza hilo kubadili wimbo huo lakini hakufanya hivyo na kila alivyoita hakuweza kutokea.

Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatato hii, Roma akiwa na mwanae, Ivan amesema anawaomba BASATA kumpungia adhabu kwani hali yake ya kiuchumi siyo nzuri.

“Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake kwa sababu muziki unamsaidia kama ajira, nyuma ya Roma kuna watu ambao anawasaidia. Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee,” alisema Roma.

Aliongeza,”Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja,

Akiwa katika mahojiano hayo na mtoto wake, Ivan aliulizwa na matangazaji wakipindi hicho kwanini hakwenda shule, na mtoto alisema hajaenda shule kutokana na tatizo la ada.

“Sijakwenda shule leo baba hana ada,” alisema Ivan mb

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PICHA:Rais Magufuli akitoa salamu za pole familia ya Kikwete

Kufuatia kifo cha Rashid Mkwachu ambaye ni Baba mzazi wa mke wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, mama Salma

Read More...

Lugola awapa maagizo wakuu wa majeshi, Wafungwa watumie nguvu zao kujitaftia chakula.

Waziri wa mambo ya Ndani, Kangi Lugola mapema leo hii ameongea na vyombo vya habari akiwasilisha maagizo mbalimbali ambayo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu