Roma yaiangamiza Barcerona na kutinga nusu fainali UEFA.

In Kimataifa, Michezo

Klabu ya Roma ya nchini Italy imeweza kuisambaratisha klabu ya Barcelona kwa kuifunga 3-0 na hivyo kutinga nusu fainali za mabingwa Ulaya kwa faida ya goli la ugenini.

Barcelona waliingia kwenye mchezo huo huku wakiwa na akiba ya magoli, ambapo kutokana na mechi ya kwanza waliyoipiga Roma bao 4-1, Roma ilikuwa inalazimika kuifunga Barcelona 3-0.

Goli la Edin Dzeko dakika za awali za mchezo (6′), na Penalty ya Daniele de Rossi katika kipindi cha pili dakika ya 58 yamekamilishwa na Goli la Mlinzi Kostas Manolas alilofunga zikiwa zimesalia dakika nane tu mechi kufikia mwisho zimewafanya Barcelona pamoja nakuwa na Lionell Messi ambaye hakufurukuta, kuondokakichwa chini katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Umati uliokuwepo Stadio Olimpico ulilipuka mara baada ya kipyenga cha mwisho pale wachezaji wa akiba wa Roma na benchi lao la ufundi walipoingia katikati ya uwanja kushangilia na wachezaji wao.

Kulikuwa na machozi katika nyuso za mashabiki wasiamini kile walichokishuhudia katika mtanange huo ambao haukutegemewa kuisha ulivyoisha.

Roma imekuwa timu ya tatu katika Champions League kuweza kuyapindua matokeo ya namna hiyo ya goli tatu au zaidi. Timu pekee mbili ambazo awali ziliwahi kufanya hivyo ni Deportivo La Coruna dhidi ya AC Milan mwaka 2004 na Barcelona dhidi ya Paris St-Germain msimu uliopita.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PICHA:Rais Magufuli akitoa salamu za pole familia ya Kikwete

Kufuatia kifo cha Rashid Mkwachu ambaye ni Baba mzazi wa mke wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, mama Salma

Read More...

Lugola awapa maagizo wakuu wa majeshi, Wafungwa watumie nguvu zao kujitaftia chakula.

Waziri wa mambo ya Ndani, Kangi Lugola mapema leo hii ameongea na vyombo vya habari akiwasilisha maagizo mbalimbali ambayo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu