Royal Tour ya Rais Samia na Mtangazaji wake

In Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuwa Royal Tour ni kipindi maarufu duniani kitakachotumika kurusha makala maalum anayoiandaa itakayoonesha vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Rais Samia ameyabainisha hayo leo Septemba 9, 2021, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

“Nimeshiriki kuandaa makala ya Tanzania itakayorushwa katika kipindi maarufu duniani cha Royal Tour, ni matarajio yangu kuwa makala hii itasaidia kuitangaza vizuri nchi yetu, kuinua utalii, kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji na kuondoa upotoshaji wa makusudi kuhusu Tanzania,” ameandika Rais Samia.

The Royal Tour ni kipindi maalum kinachotoa nafasi kwa viongozi wenye ushawishi kuonesha vivutio, utamaduni na maeneo ya kitalii ya nchi husika yanayomfanya mtazamaji wa kipindi hicho kuvutiwa na kutamani kwenda kuyatembelea, mtangazaji na mzalishaji wa kipindi hicho anaitwa Peter Greenberg.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu