Rwanda,Tanzania yaibuka vinara nchi zenye viwango vidogo vya rushwa Afrika Mashariki.

In Kimataifa, Kitaifa

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2017 iliyotolewa jana Februari 21, 2018 na Shirika la Transparency International imeonesha kuwa Rwanda ndio nchi yenye kiwango kidogo cha vitendo vya rushwa kwa mwaka 2017 ikiwa ni nchi ya kwanaza kwa Afrika Mashariki na ya pili barani Afrika ikiwa nyuma ya Botswana, ripoti hiyo imeeleza.

Tokeo la picha la Tanzania and rwanda

Ripoti hiyo imeonesha kuwa kwa Afrika mashariki, Rwanda imeongoza kwa alama 55,  Tanzania imekuwa nafasi ya pili na ya 103 duniani ambapo imepanda kutoka alama 32 mwaka 2016 hadi alama 36 mwaka 2017. Kenya imechukua nafasi ya tatu, Uganda nafasi ya nne na Burundi ikishika mkia.

Kwa bara la Afrika, nchi 10 zenye viwango vidogo vya vitendo vya rushwa ya kwanza ni Botswana, Rwanda, Namibia, Mauritius, Senegal, Afrika Kusini, Burkina Faso, Lesotho, Tunisia na ya kumi ni Ghana.

Kwa nchi kumi zilizoongoza duniani kwenye orodha hiyo nyingi ni kutoka barani Ulaya isipokuwa Canada ambayo inatoka Amerika ya Kaskazini.

Kwenye ripoti hiyo iliyohusisha nchi 180 imeonesha nchi za Afrika ndio zimeongoza kuwa na vitendo vya rushwa, ambapo kwenye nchi 10 zilizoshika mkia nchi 6 zinatoka Afrika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu